Watu 2000 Wafanya MAANDAMANO Kumuondoa MUGABE

Watu 2000 Mwishoni mwa Juma lililopita walijitokeza jijini Harare, Zimbabwe na kufanya mandamano kwa lengo la kumtaka rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 92 kuondoka madarakani.

Waandamanaji hao wanaoaminika kuwa wafuasi wa chama cha MDC wakiongozwa na kiongozi wa chama hicho Morgan Tsvangirai​ kinachompinga rais Mugabe walibeba mabango huku wakiimba nyimbo za chama .

Kwa kawaida maandamano dhidi ya serikali ya Mugabe yamekuwa yakiingiliwa kati na polisi wa nchi ya Zimbabwe.
Katika hotuba ya kiongoziwa chama cha MDC,Morgan alisema kuwa Mugabe ameshindwa kufanya ufumbuzi wa migogoro ya kiuchumi na kisiasa inayokumba taifa hilo mara kwa mara.


Rais Robert Mugabe amekuwa madarakani tangu mwaka 1980 na katika miaka ya hivi karibuni rais huyo ameonekana dhaifu kufuatia kuwa afya inayoendelea kuzorota.
Credit: trtswahili
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment