Wilbert Molandi, Dar es Salaam
YANGA imetolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika lakini
kocha wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amekiri kuwa Al Ahly
wana akili kuliko wao na hiyo ni kutokana na kile walichowafanyia kuhusu
kiungo wao, Haruna Niyonzima.
Pluijm anasema kuwa Waarabu hao waliteka mipango ambayo wao Yanga hawakuwashtukia tangu wakiwa Dar es Salaam na hivyo wakati wao wakitua Misri, tayari walishajua mbinu zao nyingi.
Pluijm anasema kuwa Waarabu hao waliteka mipango ambayo wao Yanga hawakuwashtukia tangu wakiwa Dar es Salaam na hivyo wakati wao wakitua Misri, tayari walishajua mbinu zao nyingi.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Pluijm alisema katika mechi ya pili
ambayo Yanga walifungwa mabao 2-1 juzi kwenye Uwanja wa Borg El Arab,
Alexandria nchini Misri, alipanga kufanya ‘sapraizi’ ya kumchezesha
Niyonzima akiamini Al Ahly hawamjui kwa kuwa hakucheza kwenye mechi ya
awali, lakini kumbe alikosea.
Pluijm anasema mafaili yote ya Niyonzima yalikuwa yameshafika Misri kwa kuwa mashushushu wao walibaki Dar kuifuatilia Yanga hata baada ya wao Al Ahly kuondoka baada ya mechi ya kwanza.
Pluijm anasema mafaili yote ya Niyonzima yalikuwa yameshafika Misri kwa kuwa mashushushu wao walibaki Dar kuifuatilia Yanga hata baada ya wao Al Ahly kuondoka baada ya mechi ya kwanza.
Anasema kuwa baada ya Waarabu kuondoka, Niyonzima ambaye hakucheza kutokana na kuwa majeruhi na kadi mbili za njano, alimtumia katika mechi dhidi ya Mwadui FC na dhidi ya Mtibwa Sugar, hivyo ilikuwa rahisi kwa mashushushu hao kumjua vizuri Niyonzima.
“Kwa pamoja timu yote ilicheza vizuri, tulijitahidi kumiliki safu ya kiungo tofauti na mechi ya kwanza ya Dar, lakini licha ya kuimiliki safu hiyo, kuna mipango waliiharibu Al Ahly.
“Walikuwa wameshamjua vizuri Niyonzima na yale ambayo nilipanga ayafanye mengi waliyazuia, ndipo nikajua baadaye kuwa kuna watu walibaki Dar wakiendelea kutuchunguza na walimuona akicheza.
“Walikuwa wameshamjua vizuri Niyonzima na yale ambayo nilipanga ayafanye mengi waliyazuia, ndipo nikajua baadaye kuwa kuna watu walibaki Dar wakiendelea kutuchunguza na walimuona akicheza.
“Nimeambiwa kuwa baada ya kuona michezo yetu ya Mwadui FC na Mtibwa, ndipo wakaondoka na kurudi huku (Misri) wakiwa kamili,” alisema Pluijm.
Yanga sasa itashiriki katika mechi ya mtoano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa kwenye michuano hiyo ambapo sasa imepangiwa kucheza dhidi ya Sagrada Esperança ya Angola.
Yanga sasa itashiriki katika mechi ya mtoano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa kwenye michuano hiyo ambapo sasa imepangiwa kucheza dhidi ya Sagrada Esperança ya Angola.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment