Baada
ya Tanzania na Uganda kukubaliana mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta
utekelezwe kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, matumaini mengine mapya
yameonekana kutokana na Uganda kuweka wazi azma yake ya kujenga bomba
jingine la gesi katika njia hiyohiyo kwa ajili ya biashara na Tanzania.
Licha
ya kutofafanua kwa kina juu ya mpango huo, Waziri wa Maendeleo ya
Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni aliwaambia waandishi wa habari
jana kuwa Serikali ya Uganda na Tanzania bado ziko kwenye majadiliano
ya kuanzisha mradi mwingine wa bomba hilo la gesi.
“Ni
mpango mpya bado tunajadiliana, kuna uwezekano mkubwa wa kujenga bomba
hilo lakini utekelezaji wake utaanza baada ya mradi huo wa bomba la
mafuta wa sasa kukamilika,” alisema.
Waziri
Muloni aliyekuwa ameongozana na mwenyeji wake Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo alitoa kauli hiyo katika mkutano wa
kwanza wa jopo la watalaamu wa sekta mbalimbali waliokutana kwa mara ya
kwanza kuandaa mpango wa utekelezaji wa mradi huo.
Mkutano
huo unafanyika ikiwa ni siku sita tangu azungumze na waandishi wa
habari mara baada ya kuwasili nchini akitokea Kampala ambako Rais wa
Uganda, Yoweri Museveni alitangaza kuwa bomba hilo la mafuta ghafi
kutoka Hoima, Ziwa Albert litapita katika ardhi ya Tanzania kwenda
Bandari ya Tanga.
Waziri Muhongo alisema mbali na bomba hilo, nchi nyingine za Afrika Mashariki pia zimekubali kununua gesi ya Tanzania.
Kuhusu mradi wa bomba, Profesa Muhongo alisema nchi hizo zimekubaliana kukamilisha Kazi hiyo kabla ya makubaliano ya awali ya 2020.
Kuhusu mradi wa bomba, Profesa Muhongo alisema nchi hizo zimekubaliana kukamilisha Kazi hiyo kabla ya makubaliano ya awali ya 2020.
Makubaliano
mengine ya nchi hizo ni kuchangia ujenzi wa mtambo wa kuchakata mafuta
ghafi utakaojengwa Uganda ambao alisema utasaidia kuweka akiba ya mafuta
kwa ajili ya biashara kwa nchi wanachama.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akielezea
uzoefu wa Tanzania kwenye ujenzi wa miradi ya mabomba ya gesi na mafuta
katika mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya
Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni na kulia ni Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Dk.
Fred Kaliisa (kushoto) akifafanua jambo katika kikao hicho. Kulia ni
Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene
Muloni.
Balozi wa Uganda Nchini Tanzania, Dorothy Hyuha akifafanua jambo katika mkutano huo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment