Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Shaka
Hamduni Shaka amewataka wanachama wanaojitambua kuwa ni majipu kwa
kukisaliti chama kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka jana, waanze kujitumbua
kabla hawajatumbuliwa.
Shaka alitoa rai hiyo jana katika mji wa
Orkesumet na Kata ya Ngorika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wakati
wa ziara yake ya kuhamasisha vijana kujiunga na chama hicho, kufungua
matawi mapya, kumsimika kamanda wa Kata ya Naisinyai na kukagua uhai wa
chama.
Alisema lazima wajenge chama chenye heshima na nidhamu kuliko kuwa na wanachama wasaliti ambao hawana msimamo.
Shaka alisema wanachama wa aina hiyo nyakati za asubuhi wanakuwa sehemu moja na ikifika jioni wanakwenda kwingine.
“Ni
heri wabakie wanachama wawili waadilifu kuliko wengi ambao hawana
msimamo, kufanya kosa siyo kosa, bali kosa kurudia kosa, tunajua
uchaguzi ukirudiwa tena hapa Simanjiro CCM itafanikiwa kushinda,”
alisema Shaka.
Alisema kukata tamaa ni mwiko ukiwa CCM, kwa kuwa
miaka mitano siyo mingi, hivyo wanatarajia kurudisha kata sita na Jimbo
la Simanjiro linaloshikiliwa na Chadema.
Alisema hilo litafanikiwa kutokana na uongozi bora wa Rais John Mafuguli.
“Tumesikia
wapo waliotusaliti wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, tutawachukulia
hatua, ila hivi sasa kutokana na juhudi za Rais Magufuli hata upinzani
watatupigia kura za ndiyo,” alisema.
Mwenyekiti wa UVCCM,
Wilayani Simanjiro, Kiria Laizer alisema vijana ndiyo nguvu ya chama,
hivyo kupitia jumuiya hiyo wamejipanga kukipigania na kukitetea.
“Vijana
ndiyo nguzo ya chama, tumejipanga vizuri kuhakikisha kupitia CCM,
wananchi wa eneo hili wanaendelea kukiamini na kukithamini, hivyo
tutasonga mbele,” alisema.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment