Watumishi Walioiingizia serikali Hasara Kukiona Cha Moto

Serikali imekemea na kuzitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha kwamba hazizalishi madeni yasiokuwa ya lazima na kama likitokea deni liwe deni la msingi ambalo lina umuhimu wa kuwepo kwa kujibu na kutatua hoja na shida za wananchi wake.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI George Simbachawene kwenye mkutano uliowakutanisha na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikalim za Mitaa LAAC kwenye majumuisho ya kamati hiyo ambayo ilikuwa ikihoji halmashauri 30 nchini.

Amewakanya wakurugenzi na maafisa fedha wa halmashauri nchini waache mara moja tabia ya kuandika madeni ya uongo ili wajipatie fedha kwa njia isiyo halali ambayo inawasababishia watanzania kukosa haki zao za msingi hasa zile za kuwasaida katika kupata huduma mbalimbali.

Amesema serikali imeanza kuhakiki madeni halali na kuanza kuyalipa na kwa yale ambayo sio halali kulipwa na serikali watawajibishwa watendaji husika hata kama kwa sasa hawapo kazini kwani serikali ina mkono mpana wa kuwachunguza wabadhirifu na kuwachukulia hatua mbalimbali kisheria.

Amesema kauli ya serikali kwa wakurugenzi ambao watahusishwa na ubadhirifu wa fedha na walioshindwa kujibu hoja za mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali ofisi yake itachukua hatua stahiki katika kuwawajibisha wakurugenzi hao waliohusika kwa namna moja ama nyingine.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment