MOISE
Katumbi Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga, Mkurugenzi wa klabu ya TP
Mazembe na mfanyabiashara marufu nchini Kongo ametangaza kugombe urais
wa Novemba mwaka huu.
Muungano
wa vyama kadha vya upinzani umemuidhinisha Katumbi kuwa mgombea huku
muungano huo ukiwa umegubikwa na hofu ya huenda Rais Joseph Kabila
akaendelea kushikiri madaraka kinyume na katiba hiyo.
Katumbi
amekuwa Gavana wa jimbo la Katanga tangu 2007 chini ya chama cha
People’s Party for Reconstruction and Democracy(PPRD) na baadae
akajiuzulu nafasi hiyo septemba 2015 ambapo mwaka huu 2016 amekuwa
akitoa kauli zinazo mtaka Kabila kuheshimu katiba ya taifa hilo inayo
mtaka kustaafu mwishoni mwa mwaka huu.
Licha
ya Katumbi kumsaidia Kabila katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2006 na
2011 kwasasa anaonekana kuwa mbali na kiongozi huyo tangu kujiuzulu
kwake 2015.
Hata hivyo mfanyabiashara huyo amekuwa na umaarufu mkubwa kutokana na kumiliki klabu ya TP Mazembe tangu 1997.
Uchaguzi
huo unaonekana kuwa na mchuano mkali kwa kuwa Katumbi ana nguvu kubwa
ya kiushindani kuanzia katika jimbo la katanga na katika ngazi ya taifa
licha ya kukabiliwa na tuhuma za ubadhilifu wakati wauongozi wake.
Wachunguzi
wa habari za siasa wamesema nchi hiyo inanyemelewa na machafuko iwapo
Rais Kabila atataka kuendelea kuongoza taifa hilo kwa nguvu kama ilivyo
fanyika Burundi na Rais Nkurunzinza.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment