Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Boniface Jacob ametangaza
kumsimamsha kazi mwanasheria mkuu wa manispaa hiyo, Burton Mahenge na
Mthamini wa Manispaa Einhard Chidaga.
Uamuzi huo umechukuliwa kwa kauli moja na madiwani wa manispaa hiyo kufuatia kikao chao mwishoni mwa mwezi uliopita.
Mheshimiwa
Jacob amewaeleza waandishi wa habari kuwa wawili hao wameisababishia
hasara kubwa, kupoteza mali, na kuchelewa kupata manufaa katika mali
zake.
Makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo ni:
1. Miradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa.
Manispaa
ilipaswa kupata shilingi Milioni 900 kwa mwaka kwa uwekezaji huo.
Lakini kutokana na mgogoro wa kimkataba Mapato hayajawahi kulipwa hivyo
kupoteza shilingi Bilioni 4.5 mpaka sasa.
2. Mgogoro wa wapangaji wa Nyumba za Magomeni Kota.
Manispaa
iliandaa mpango wa kuendeleza eneo la Magomeni Kota, hivyo kuwaondoa
wapangaji hao na kubomoa Nyumba hizo longer, wapangaji walifungua shauri
la kupinga kuondolewa katika Nyumba na kutoa madai ya kujengewa nyumba
ama kulipwa fedha za fidia kutokana na Usimamizi hafifu wa shauri hili
Mahakama liamuru Manispaa kukaa na kumalizana na wapangaji nje ya
mahakama.
Halmashauri
ikatengeneza mkataba wa kuwalipa wapangaji kiasi cha shilingi
1,080,000/= kwa kila mpangaji kama kodi ya mwaka na kumpatia kila
mpangaji kiwanja. Hivyo Manispaa inatakiwa kulipa shilingi
3,271,520,000/= kugharamia fidia hiyo kwa mchanganuo wa shilingi
695,520,000/= pango la mwaka na 2,576,000,000/= fidia ya viwanja 644.
3.Uwekezaji eneo la Coco Beach Oysterbay
Manispaa
iliingia mkataba na Q - Consult Limited, Kampuni hiyo ilishindwa
kutekelezwa mradi kwa wakati na Manispaa ikavunja Mkataba huo. Q-Consult
Limited ilifungua shauri ambalo halikusimamiwa vizuri na kwa sababu ya
kutofika kwenye kesi, Manispaa ilipoteza kesi hiyo.
Halmashauri iliagiza kukata kwa rufaa lakini haikuwa na hatua zozote zilizochukuliwa na hivyo Manispaa inaweza kupoteza haki yake. Iliagizwa na Serikali Mwanasheria Mkuu baada ya tamko la Rais Mhe. John Pombe Magufuli kutangaza nia ya kutoachia eneo hilo mpaka sasa Mwanasheria alikuwa hajakata rufaa.

4.Mradi wa Ujenzi wa maduka Makumbusho (Eastern Capital Ltd)
Mkataba juu ya uendeshaji wa stendi haina manufaa kwa Halmashauri ,KMC inapata 1% ya makusanyo kwa mwaka sawa na Shilingi Milioni 4 tu kwa mwaka, wakati kabla ya uwekezaji, local standy Halmashauri ilikuwa ikipata Milioni 12 kwa mwezi.

5. Kubomolewa kwa ofisi ya Kata ya Msasani.
Mwananchi
ajulikanaye kwa jina la Chacha aliingilia eneo la ofisi ya kata ya
Msasani na baadae kuishtaki Manispaa. Usimamizi dhaifu wa shauri hilo
kuisababishia mahakama kutoa amri ya kubomoa ofisi ya Kata, Manispaa
imekata rufaa na sasa ni muda mrefu shauri halisikilizwi na hakuna
ufuatiliaji unaendeleaje.
Hata hivyo kwa makusudi Bw. Chacha aliamua kuuza Kiwanda hili kwa Lake Oil CO. Limited wakati shauri halijaisha.
Manispaa imekosa manufaa mengi kwa kuchelewa kukamilika kwa shauri hilo, yangu upande wa pili ulikataa Jaji, tuna zaidi ya mwaka hatujapangiwa Jaji mwingine na hatujafuatilia kama Halmashauri.

6.Ujenzi wa Nyumba za makazi (Apartment) Hill Road Oysterbay.
Mradi
inafanyika kwa ubia na mwekezaji Texas Enterprise Company Ltd, mkataba
uliingiwa mwaka 2009, na mradi umesimama kwa muda mrefu sasa.
Pamefanyika mabadiliko katika mkataba na mkataba umefanyiwa marekebisho bila idhini ya Halmashauri. Manispaa inakosa manufaa ya mali yake kwa sababu ya kuchelewa kwa mradi. Lakini pia uendeshaji mpya wa sasa hauna makubaliano wa Financial proposal na Investment capital.

7. Ujenzi wa Nyumba za makazi (Apartment s) Kiwanda no. 314 Toure Drive.
Mradi huu unatekelezwa kwa ubia na Kampuni ya Lake Oil Limited mkataba uliingiwa 2009.
Mabadiliko
yamefanyika katika Mkataba bila idhini ya Halmashauri na kuisababishia
mradi kuchelewa kukamilika, Manispaa inakosa manufaa ya mali yake kwa
kuchelewa kukamilika mradi.
Halmashauri bado inaendelea kufuatilia miradi mwingine ambayo umeingia na haina manufaa kwa Halmashauri.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment