SERIKALI
imekanusha madai ya kutoa maelekezo kwa Uongozi wa vyuo vya elimu ya
juu ya kuwanyanyasa wanafunzi wa vyuo hivyo wanaojihusisha na masuala ya
siasa na badala yake imewataka wafuate kanuni na taratibu zilizowekwa
sehemu husika.
Hata
hivyo imesema itaendelea kuwahudumia Watanzania wote ikiwemo kutoa
elimu kuanzia ngazi awali hadi elimu ya juu bila kujali ya itikadi za
dini wala vyama vyao vya siasa.
Waziri
Mkuu,Kassm Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 5, 2016) wakati
akijibu swali la papo kwa papo la Mheshimiwa Ester Matiko (Viti maalum
Chadema) aliyetaka kujua kama Serikali imetoa maelekezo kwa uongozi wa
vyuo vikuu kunyanyasa wanafunzi wanaojihusisha na masuala ya siasa.
“Nakanusha
si kweli kwamba kuna maelekezo kwenye vyuo vyote vya elimu ya juu na
pia hakuna unyanyasaji wowote wa vyuo na Watanzania wote wanao uhuru wa
kujiunga na vyama vyote wanavyovitaka, lakini kila eneo limeweka
utaratibu wake hivyo wafuate taratibu na sheria katika sehemu husika,” alisema.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imeondoa tozo ya asilimia
15 ya eneo la manunuzi ya vifungashio katika zao la korosho ili kumfanya
mkulima kupata tija zaidi.
Akijibu
swali la papo kwa papo la Mheshimiwa Katani Katani (Tandahimba-CUF)
aliyetaka kujua ni lini tozo hiyo itaondolewa, Waziri Mkuu Majaliwa
amesema tayari tozo hiyo imeshaondolewa na gharama hizo kwa sasa zipo
katika mfuko wa wakfu ulioundwa na wadau wa zao hilo na unachangiwa na
asilimia 65 ya tozo za korosho zinazouzwa nje.
Amesema
mfuko huo wa wakfu unatakiwa kusimamia upatikanaji wa masoko ya zao la
korosho, kununua pembejeo, kusimamia uboreshaji na upanuzi wa mashamba
na kugharamia tatifi mbalimbali kwa ajili ya kupata ubora wa zao hilo.
Akijibu
kuhusu suala la madai ya wakulima ambao korosho zao zimepotea ghallani,
amesema mfumo wa uuzwaji wa zao hilo wa stakabadhi ghalani ni wa
kiushirika na unasimamiwa na Mrajisi ni vema wakulima wakadai haki yao
katika mikutano ya ushirika wao na kama hawaridhiki na majibu waende
mahakamani ili kupata haki yao.
Amesema
kwa sasa Serikali itahamishia nguvu zake katika kusimamia mazao mengine
ya pamba, tumbaku na kahawa kama walivyofanya kwenye zao la korosho ili
wakulima wa mazao hayo nao wapate tija.
Akijibu
swali la Mheshimiwa Joseph Kekunda (Sikonge-CCM) aliyetaka kujua
Serikali inampango gani wa kutatua migogoro ya wakulima na wakulima
,Waziri Mkuu amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali katika
kuhakikisha inakomesha migogoro hiyo ambazo ni pamoja na kupima maeneo
na kuweka mipango bora ya matumizi ya ardhi.
Pia
kuweka mipaka katika maeneo mapya na kutumia ranchi zilizopo kwa ajili
ya wafugaji wakubwa na kwamba itatenga maeneo ya kilimo na kuyabainisha
kwa wananchi ili kuepuka muingiliano uliopo hivi sasa
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment