Tamko la RC MAKONDA Kuhusu Mashoga Waliopo Jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza vita na makaka poa (mashoga) na madada poa (makahaba) walioko jijini Dar es Salaam kuwa utaendeshwa msako mkali wa kuwaondoa.

Mkuu wa Mkoa huyo aliyasema hayo kufuatia hali ya vitendo hivyo visiyokubalika na jamii kuzidi kushamiri na kuwa kuna hatari kubwa ya watoto wadogo kuiga vitendo hivyo vinavyoleta picha mbaya kwani ni kinyume na maadili ya mtanzania.

Aidha alisema hawezi kuifumbia macho hali hii kwani inamomonyoa maadali ya jamii na kuwa yuko tayari kulivalia njuga suala hili ili kuhakikisha anawamaliza wote mkoani

Sakati hili la ushoga na ukahaba limeibuka siku za hivi karibuni baada ya kituo cha televisheni cha Clouds Tv kumhoji shoga mmoja ambapo jamii ilipinga kitendo hicho na kuona kama walikuwa wakiuhalalisha ushoga na kuaminisha jamii kuwa ni kitu kizuri.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment