Mrisho NGASSA Kavunja Mkataba na Klabu Yake ya South Afrika

Winga mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaichezea klabu ya Free State ya Afrika Kusini Mrisho Khalfan Ngassa leo September 1 2016 ameripotia kuamua kuvunja mkataba na klabu yake ya Free State.

Kwa mujibu wa barua ambayo inaonesha kuwa Ngassa kwa sasa ni mchezaji huru na anaruhusiwa kucheza katika klabu yoyote, imeeleza kwa kifupi kuwa Ngassa amevunja mkataba na Free State toka August 25 2016.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mrisho Ngassa alijiunga na Free State kwa mkataba wa miaka minne, hiyo ni baada ya kuondoka Yanga kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu wa 2014/2015 na amedumu nayo kwa kipindi cha mwaka mmoja

TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment