Taarifa zilizotoka mkoani humo zimedai kuwa tetemeko hilo halikuwa kubwa tofauti na lile lililotokea siku ya Jumamosi na kusababisha vifo vya watu 16 na wengine 253 kujeruhiwa, nyumba 840 kubomoka na nyingine 1264 zikibakia na nyufa.
Wakati huo huo mabweni ya shule ya sekondari ya Nyakato yakiharibika kabisa na kusababisha wanafunzi wa shule hiyo kukosa mahali kwa kulala.
Awali akiongea baada ya kutembelea waathirika wa tetemeko hilo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliwataka wakazi ambao nyumba zao zimeharibiwa kutorejea tena wenye nyumba hizo kutokana na kutofahamika kama tetemeko hilo lingerudi kwa mara nyingine.
“Tuna wasiwasi kuwaingiza tena kwenye mabanda yale, tukiwalaza tena hapo halafu kama litarudi tena jioni tunaweza kuwa na hadithi nyingine tena mbaya sana. Mtatuvumilia, tuombe muwatumie wataalamu wetu wa hali ya hewa na wengine wanaofanya kazi ya kuangalia shughuli zilizopo chini ya ardhi, kama huu mtikisiko ni endelevu au umekuja kwa muda mfupi,” amesema Waziri Mkuu.
Aidha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amehirisha ziara yake ya siku tatu nchini Zambia ikiwemo kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais wa sita wa nchi hiyo, Edgar Lungu kwa ajili ya kufuatilia maafa hayo yaliyotokea mkoani Kagera na kumuagiza Mama Samia Suluhu kumwakilisha kwenye ziara hiyo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment