Jenerali Athanase Kararuza.
OFISA Mkuu wa Jeshi la Burundi, Jenerali Athanase Kararuza ameuawa
pamoja na mkewe baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana
mjini Bujumbura leo asubuhi.
Jenerali Kararuzana na mkewe wameuawa katika Tarafa ya Mutanga
wakiwapeleka watoto wao shuleni, ofisa mmoja wa usalama ambaye hakutaka
jina lake litajwe ameliambia shirika la habari la AFP.
Wizara ya ulinzi pia imethibitisha kifo cha jenerali huyo.
Athanase Kararuza alikuwa mshauri wa masuala ya ulinzi katika ikulu
ya rais na kamanda wa pili katika kikosi cha kimataifa cha kulinda amani
Jamhuri ya Afrika ya Kati.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment