Mashabiki wa Arsenal wamemshambilia meneja wa timu hiyo Arsene Weger katika mtandao wa twitter na kumtaka aondoke na nafasi yake ichukuliwa na raia wa Argentina, Diego Simeone.
Wamesisitiza kuwa timu ya Arsenal chini ya Wenger haijatwaa ubingwa wa Ulaya tangu mwaka 2004 na wala haijashinda UEFA Champions League hata mara moja.
Aidha mashabiki hao walimkubali zaidi Diego Simeone baada ya kuiongoza vyema klabu yake ya Hispania Atletico Madrid na kufanikiwa kuwafunga vigogo wa Ujerumani Bayern Munich 1-0 katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya UEFA.
Kambi ya Wenger msimu huu imetikisika kwa kias kikubwa kutokana na shinikizo kutoka kwa wadau wa klabu hiyo na kusababisha kuharibika kwa mbio zao za ubingwa walizoanza vyema.
Diego Simeone
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment