Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven amemwagiza Kamanda wa Polisi mkoa huo,
Jacob Mwaruanda kuwasaka na kuwakamata watumishi hewa 18 waliobainika
katika uhakiki uliofanyika katika halmashauri zote mkoani humo hivi
karibuni.
Pia ameagiza fedha hizo zilizolipwa kwa watumishi hao hewa na kuiingizia hasara kubwa Serikali zirudishwe mara moja.
Akifafanua
alisema katika uhakiki huo, watumishi hewa tisa walibainika katika
wilaya ya Nkasi, wanane katika Manispaa ya Sumbawanga na mmoja wilaya ya
Sumbawanga wakati Kalambo ikiwa haina mtumishi hewa.
Uhakiki
huo unatokana na maagizo aliyotoa Rais John Magufuli baada ya
kuwaapisha wakuu wa mikoa aliowateua, aliwaambia wakafanye kazi ya
kutatua kero za wananchi na sio kwenda kufanya siasa.
Pia
Rais Magufuli aliwapa wakurugenzi wa halmashauri siku 15 wawatoe katika
orodha ya malipo ya mshahara wafanyakazi hewa wote katika halmashauri
zote nchini.
Zelothe
alitoa agizo hilo jana katika kikao maalumu cha kufahamiana
kilichojumuisha wazee , viongozi wa dini , watendaji wa umma na wajumbe
wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo kilichofanyika mjini hapa.
Alisisitiza kuwa hajaridhishwa na uhakiki huo, hivyo akaagiza halmashuri zote kurudia upya uhakiki wa watumishi.
Alisisitiza kuwa hajaridhishwa na uhakiki huo, hivyo akaagiza halmashuri zote kurudia upya uhakiki wa watumishi.
“Siku
ile ile nilipoapishwa kabla sijavuka geti kutoka nje ya Ikulu nilipiga
simu na kuagiza halmashauri zote (Manispaa, Nkasi, Kalambo na
Sumbawanga) kuanza uhakiki mara moja wasinisubiri hadi niripoti mkoani
hapa,” alieleza.
Aliongeza
kuwa aliporudi mkoani humo na kuripoti kazini katika siku yake ya
kwanza ofisini alikabidhiwa kitabu chenye orodha ya watumishi wa umma wa
halmashauri zote akielezwa kuwa hakuna mtumishi hewa katika mkoa wa
Rukwa.
“Sikukubaliana
nao nilikataa, nikaagiza ufanyike uhakiki mara moja ndipo wamepatikana
watumishi hewa 18 na watumishi wengine 137 wapowapo tu wakiwa na taarifa
zinazotia mashaka. Wote wamebainika kwenye hicho kitabu
nilichokabidhiwa kikionesha hakuna mtumishi hewa,” alisisitiza.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment