KAPTENI wa Timu ya Taifa ya
Brazil anayekipiga kunako Klabu ya Barcelona ya Hispania, Neymar Dos
Santos mwenye umri wa miaka 24 ameweka wazi kuwa ataendelea kubaki
klabuni hapo kwa miaka mingine mitano ijayo.
Neymar aliyekuwa akihusishwa kujiunga na Klabu ya Paris Saint-Germain
(PSG) kwa dili kubwa zaidi amesema kuwa anapenda kuendelea kuichezea
Barca na hiyo ndiyo imekuwa ndoto yake ya miaka yote kuwatumikia magwiji
wa Catalan.
Rais wa Barcelona, Josep Bartomeu amesema Neymar
amekubali dili jipya la kubaki klabuni hapo na atakamilisha taratibu za
kusaini siku za usoni huku akiongeza kuwa watamchukua pia Samuel Umtiti wa Lyon kwa paun euro milioni 20.
Neymar alijiunga na Barca mwaka 2013 akitokea klabu ya Santos ya Brazil na ameisaidia Barca
kunyakuwa ubingwa mara kadhaa ambapo msimu uliyoisha Mei, Barcelona
ilinyakuwa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania (LaLiga) 2016/17.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment