Omary Mdose na Nicodemus Jonas
USHINDI iliyoupata TP Mazembe ya
DR Congo dhidi ya Yanga, Jumanne ya wiki hii, umevunja rekodi ya Yanga
ya kutofungwa kwenye uwanja wake wa nyumbani kwa takribani miaka sita
iliyopita katika michuano ya kimataifa inayosimamiwa na Shirikisho la
Soka la Afrika (Caf).
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar, Yanga ilifungwa bao 1-0 katika mchezo wa Kundi A
katika Kombe la Shirikisho Afrika, ikiwa kundi moja na timu nyingine za
Medeama ya Ghana na MO Bejaia ya Algeria
Rekodi zinaonyesha kuwa, mara ya mwisho
Yanga kufungwa nyumbani katika michuano hiyo na ile ya Ligi ya Mabingwa
Afrika ilikuwa ni mwaka 2010 ambapo ulikuwa ni mchezo wa Ligi ya
Mabingwa Afrika dhidi ya timu ya Saint Eloi Lupopo ya DR Congo.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Dar, Yanga ilifungwa mabao 3-2, mchezo wa pili nchini DR Congo, Yanga ikafungwa tena bao 1-0.
Yanga ipo chini ya mwenyekiti wake Yusuf
Manji ambaye ana uwezo mkubwa wa kifedha wakati Mazembe inamilikiwa na
Moise Katumbi ambaye naye ni mmoja wa matajiri wa DR Congo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment